Monday - Friday ( 08:00 AM - 04:30 PM )
ATEATEATE
+255 22 2780023
info@ate.or.tz
Mikocheni Industrial Area, Dar es Salaam

Waziri Ndalichako afanya ziara Ofisi za ATE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako (Mb) akiambatana na Naibu Waziri katika Wizara hiyo Mheshimiwa Patrobas Katambi (Mb) Jumanne tarehe 25 Januari 2022 alitembelea katika Ofisi za Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dar es Salaam kwa mazungumzo na utambulisho.

Mhe. Waziri amefanya mazungumzo na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya ATE ikiongozwa na Mwenyekiti Bi. Jayne Nyimbo pamoja na Menejimenti ya ATE ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Suzanne Ndomba- Doran.

Katika hotuba yake Mhe. Waziri ameipongeza ATE kama mdau wa UTATU kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa Wizara hiyo katika kuboresha Sekta  ya ajira na kazi nchini  na kuwasisitiza waajiri wote nchini ambao bado hawajajiunga na ATE kufanya hivyo ili kufaidika na huduma za ATE

Katika salamu zake Bi. Suzanne Ndomba amemshukuru Mh. Waziri na ujumbe wake kwa kutembelea Chama cha Waajiri katika siku zake za awali katika Wizara hiyo lakini pia alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuigawanya Wizara na kuitenganisha na Sera, Bunge na Uratibu kwani italeta wepesi wa kiutendaji katika masuala ya kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.