Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) siku ya Jumamosi tarehe 5 Novemba 2022 walifanya Bonanza la Michezo “Waajiri Health Bonanza “ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako ( MB). Katika hotuba yake Mh. Waziri amewapongeza ATE kwa kuandaa bonanza hilo lenye malengo ya kuhamasisha na kuelimisha umuhimu wa usalama na afya mahala pa kazi kwa ustawi wa biashara.
Katika salamu zake Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba – Doran ameeleza kwamba hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa bonanza hilo na kwamba litakua likifanyika kila mwaka ili kuendelea kutoa hamasa kwa waajiri kuhusu masuala ya afya na usalama katika maeneo ya kazi. Bi. Ndomba- Doran aliongeza kuwa kwa mwaka huu Makampuni 129 wameshiriki, ambapo makampuni 49 walifika Viwanja vya Leaders na kuonyesha biashara zao. Michezo mbalimbali na mazoezi yamefanyika oamoja na burudani kutoka bendi ya Walemavu inayoitwa Tunaweza Band.
Bonanza hilo lililobeba kauli mbiu isemayo “Wanyakazi wenye afya ni mtaji” liliandaliwa na ATE na kudhaminiwa na ILO, UNAIDS, OSHA, Coca Cola, SGA Security na Hospitali ya Kairuki.