Uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Mwanamke Kiongozi kwa Wabunge Wanawake
ATE yazindua Programu ya Mafunzo ya Mwanamke Kiongozi (Female Future) kwa Wabunge Wanawake yanayoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri la Norway ( NHO) ulifanyika rasmi leo katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni Dodoma ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai (Mb) akiambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh. Jenista Mhagama( Mb). Hafla hii pia ilihudhuriwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wadau wa ATE wakiwemo Shirika la Kazi Duniani (ILO) Ubalozi wa wa Norway nchini na Chuo cha Uongozi ESAMI