Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Siku ya Alhamisi tarehe 22 Juni 2023, kilianya Mkutano wake Mkuu wa 64 ambao pamoja na mambo mengine uliambatana na uchaguzi wa viongozi katika nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambao wataongoza ATE kwa miaka mitatu(3) – 2023-2026.
Katika uchaguzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) Bw. Oscar Mgaya alichaguliwa na Mkutano Mkuu kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE ) ambaye aliwashukuru wanachama kwa kumchagua kushika nafasi hio na kuahidi kushirikiana na viongozi wenzake kuyaendeleza mazuri yote yaliyoachwa na viongozi waliomaliza muda wao na pia kuomba ushirikianao kutoka kwa waajiri, Serikali na Vyama vya Wafanyakazi kwa manufaa ya ukuaji wa sekta ya ajira na kazi nchini.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi Mkazi wa G4S Secure Solutions (T) Limited Bi. Imelda Lutebinga, alichaguliwa na Mkutano Mkuu kushika nafasi hio ambaye nae aliahidi kushirikiana na viongozi wenzake katika kuongoza ATE iweze kusonga mbele zaidi.
Viongozi waliochaguliwa lwataongoza ATE kwa kipindi cha Miaka 3 kama ambavyo katiba ya ATE inaelekeza.