Monday - Friday ( 08:00 AM - 04:30 PM )
ATEATEATE
+255 22 2780023
info@ate.or.tz
Mikocheni Industrial Area, Dar es Salaam

ATE yafanya Mkutano wa 5 wa Uongozi ulioambatana na Mahafali ya Programu ya Mwanamke Kiongozi

Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) siku ya Machi 10 Machi 2023 imefanya Mkutano wa 5 wa Uongozi ulioambatana na Mahafali ya Programu ya Mwanamke Kiongozi (Female Future Programme) ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), aliyeambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb), Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) pamoja Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Uchumi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake Zanzibar (UWAWAZA), Mhe. Dkt. Saada Mkuya.

Mada kuu ya mkutano wa mwaka huu ni “Mchango wa Mabadiliko ya Kidijitali katika Kuimarisha Usawa wa Kijinsia katika Uchumi wa Tanzania: Mafanikio, Changamoto na Fursa” Unaoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani kwa mwaka 2023 ambayo imejikita katika kuangazia ushiriki wa wanawake katika mabadiliko ya kidijitali.

Akizungumzia mada kuu ya mkutano huu, Mhe. Waziri Mkuu amesema kwamba kila mmoja wetu anapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko ya Kidijitali kwa maendeleo ya Uchumi wetu na Taifa kwa ujumla. 

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri Mkuu, amewasisitiza kuendelea kutoa mafunzo katika maeneo ya Uongozi na kuwasisitiza Wanawake kuendelea kujifunza ili kuwa na uelewa wa juu katika mambo ya kidijitali.

Sambamba na maagizo mengine Mhe. Mgeni Rasmi amewasisitiza waajiri nchini kuboresha mifumo yao ya Kidijitali ili kurahisisha utendaji katika maeneo yao ya kazi hadi kuifanya nchi kufikia hatua ya kuongozwa kidijitali. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran akitoa salamu za ukaribisho amesema kuwa malengo ya programu hii ni kuwaongezea ujuzi wanawake katika uongozi ili waweze kumudu nafasi za juu za uongozi na kueleza kuwa katika programu hii inayotolewa kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi cha ESAMI, washiriki wanafundishwa Uongozi (Leadership), Rhetoric (mawasiliano) na Board Competence (umahiri katika bodi) na kubainisha kuwa mpaka sasa jumla ya wanawake 274 kutoka katika makampuni 79. 

 

Mkutano huu umehudhuriwa pia na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Elisabeth Jacobsen, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani kwa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda & Burundi, Bw. Wellingtone Chibebe, Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Shally Josepha Raymond (Mb), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina, Mtendaji Mkuu wa ESAMI, Professor Martin M. Lwanga na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ATE. 

Wengine waliohudhuria ni Wakurugenzi na Maafisa Watendaji Wakuu wa Taasisi mbalimbali,Wadau wa Utatu kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, wahitimu wa Awamu ya Nane ya Mafunzo ya Programu ya Mwanamke Kiongozi pamoja na wadau  wa maendeleo kutoka hapa nchini.