Monday - Friday ( 08:00 AM - 04:30 PM )
ATEATEATE
+255 22 2780023
info@ate.or.tz
Mikocheni Industrial Area, Dar es Salaam

ATE yafanya Mkutano wa 4 wa Uongozi ulioambatana na Mahafali ya Saba (7) ya Programu ya Mafunzo ya Mwanamke Kiongozi.

Dar es salaam,

Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri la Norway (NHO) siku ya tarehe 2 Machi 2022 kimefanya Mkutano wa 4 wa Uongozi ulioambatana na Mahafali ya Programu ya Mafunzo ya Mwanamke Kiongozi (Female Future Programme) ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango aliyewakilishwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) aliyeambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb).

Mkutano huu uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Dar es salaam umebeba ujumbe unaosema “Usimamizi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi: Usawa kwa Maendeleo ya Sasa na ya Baadae” ambayo imejikita katika kuangazia ushiriki wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kujadili namna yanavyoathiri wanawake na namna gani wanashiriki katika usimamizi wa mabadiliko ya tabia nchi kwa maendeleo endelevu ya Taifa na dunia kwa ujumla.

Lengo la Mkutano huu ni kukutanisha viongozi na wadau mbalimbali kujadili juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi.

Kwa upande wa Mahafali ya Awamu ya 7 ya Mafunzo ya  Programu ya Mwanamke Kiongozi Jumla ya Wanawake 43 kutoka katika Makampuni 23 na wengine 7 waliojidhamini wenyewe wamehitimu katika mafunzo haya yenye lengo la kuwajengea wanawake uwezo  ili waweze kushika nafasi za Juu za Uongozi.