ATE yaungana na Dunia kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani
Katika kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani Disemba 1 mwaka huu, Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na ILO na PSI Tanzania iliendesha zoezi la kuelimisha wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered kuhusu Upimaji wa VVU mahali pa kazi kwa kutumia kipimo binafsi cha JIPIME kwa lengo ni kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora na salama katika maeneo ya kazi.
Maadhimisho ya Mwaka huu yalibebwa na Kauli mbiu isemayo “Zingatia Usawa, Tokomeza UKIMWI, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”