Monday - Friday ( 08:00 AM - 04:30 PM )
ATEATEATE
+255 22 2780023
info@ate.or.tz
Mikocheni Industrial Area, Dar es Salaam

ATE yafungua Rasmi Ofisi ya Kanda ya Kati Dodoma

Chama cha Waajiri Tanzania( ATE) siku ya Jumanne tarehe 9 Novemba 2021 kilifanya mkutano na Waajiri Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya ufunguzi rasmi wa Ofisi zake kwa ya Kanda ya Kati.

Akizungumza katika Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE Bi. Suzanne Ndomba-Doran alisema lengo ni kuwa karibu na Waajiri na pia kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamishia shughuli zake jijini Dodoma ikizingatiwa ATE ni mmoja wa Wadau wa UTATU wa Shirika la Kazi Duniani. Pia akaongeza kuwa Ufunguzi wa Ofisi za Kanda ni utekelezaji wa matakwa ya Katiba ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).